Zua Rabsha

Kulikuwa na punda wawili , mmoja mnene na mwingine mwembamba kiasi. Wote walikuwa wakila nyasi katika eneo mmoja. Yule mnene alipoishiwa na nyasi akaenda kunyemelea kwa mwenzake na kuzua rabsha. Punda mwembamba alisema yeye ni kwanza hapo na hajala cha kutosha. Punda mnene alikataa kusikia na kumfukuza kwa nguvu akitumia mateke.

Punda mwembamba alianza kupiga kelele na kufanya mwenye boma kufika pale. Lakini alipofika alipata kuwa simba ametangulia. ‘Simba amefika pia!’, Binadamu akatamka. ‘Sasa itakuwa aje?. Mimi nahisi njaa.’,simba akasema.

Baada ya kuwaza Binadamu akamwambia kwanza azungumze na punda wawili wake. Yule mnene akamwambia kwamba atampaka rangi ya mistari kama nyasi na kumwachilia huru aende kuishi msituni. Yule mwembamba akamwambia atabaki naye kwa boma na atapata lishe kutoka kwake. Punda wote wawili waliridhishwa na uamuzi wake. Wa kwanza alipopakwa rangi akakimbia msituni.

Binadamu akamweleza Simba kuwa amebaki na yule mwebamba na yule mnene ametorokea kichakani ambapo simba hakuwa na budi kumtafuta yule mwingine. Kutokea hiyo siku punda huyo mnene wa kulia na marangi akabandikwa jina pundamilia.