Uongo kwa sauti kubwa

sauti kubwa

Itakuwaje kama kila mmoja atatangaza mambo yake hadharani?Kama wote wapo kwenye nyumba moja hakutakalika. Serikali ni moja. Hata kwa bongo serikali ni hiyo moja.

‘Tuseme wewe Tekepunda ndio serikali hapa’, Rasto akasema.

‘Sisi wengine hapa ni kusema tu’, Boflo akaongeza.

‘Kumbuka hayo maneno ndio yatakayo kuingiza kwa shida.’,Tekepunda akawaambia.

‘Rasto ndiye aliyempigia simba simu.’, Boflo akajitetea akielekeza kidole kwa Rasto.

‘Maji yakisha mwagika hayazoleki.’, Tekepunda akarudisha.

‘Sasa tufanye nini?’,Rasto akauliza kwa sauti.

‘Tusubiri hapa. Hakuna lingine la kufanya.’