Hapo zamani za kale

jogoo na panzi
jogoo na panzi

Mende akamwambia mwenzake kipepeo ,’Tufanyeje?’

‘Kwa nini?’, akauliza kipepeo.

‘Wewe huoni? Jogoo wanapigana!.’, akasema huku akielekeza kidole kwenye jogoo hao wawili ambao walikuwa wakipigana.

‘Wewe unataka tujiingize kwa vita baina ya jogoo wawili?, kipepeo akaulizwa.

‘Unaelewa kile wanachopigania? Wacha wakwaruzane na kama macho yako yanaumia pole.’, kipepeo akaongeza.

‘Macho kweli hayana pazia.’, mende akalia.

‘Ni kweli lakini kumbuka amani wakati mwingine haiji bure.’, kipepeo akaeleza.