Watetea ndizi na mgomba si wako

ndizi kuanguka

“Nilikupa ndizi  ukakataa. Angalia sasa tuko kotini. Mbona hivi?”, Paka akamwuliza Kunguru.

‘Mimi nilikuwa naelekea sokoni ndiposa nikakuona ukibeba ndizi’. Kunguru akajibu.

‘Wewe umewahi kuona paka akila ndizi?’, Paka akauliza.

‘Kusema kweli sijawahi kouna hata paka mmoja akila ndizi.’, Kunguru akajibu.

‘Mbona waniwekelea mambo kama haya. Mambo ambayo hayaeleweki?’, Paka akauliza tena.

‘Mimi nilikuona ukichuma ndizi  ukiweka ndani ya gunia. Kubali wewe ni mwizi !’, Kunguru akasema kwa sauti.

‘Duh! Unahakika ni mimi uliona? ‘, Paka akauliza kwa ukali.

‘Ni wewe. Hata hivyo nilikuonya.’ , Kunguru akajibu.

‘Sasa wewe watetea ndizi na mgomba si wako.’, Paka akarudisha.

‘Uko na swali lingine?’, hakimu Twiga akauliza Paka.

‘Ni hayo tu mheshimiwa.’, Paka akajibu.