Mwenye shibe hamjui mwenye njaa

tumbo

Tumbili alipandishwa kizimbani pamoja na Paka. Paka akiwa na majeraha madogo madogo kichwani kutokana na kichapo alichopata akiwa anatoroka  naye Tumbili alikuwa ameshika mkia wake.

‘Inasemekana kuwa mimi ndiye nilituma paka. Wewe ulinionea wapi?’, Tumbili akauliza Kunguru.

‘Mimi sikukuona lakini…’, Kunguru akakatizwa na Tumbili.

‘Kweli hukuniona. Sasa unasema nini na hapa tuko kotini?’ , Tumbili akauliza akiwa amenyoosha mikono yake kama bila makosa.

‘Wewe mjanja sana.’, Kunguru akasema.

‘Ulijua kwamba wengine wangekushuku kama wangekuona shambani ndiposa ukamtuma Paka.’, Kunguru akaongeza.

‘Wacha nikurekebishe. Tumbili alinidanganya kuwa shamba ni lake.’ Paka akafoka.

Kelele likazidi kotini.

‘Nyamazeni na mtulie. Tuko kotini.’, hakimu twiga akawaambia wote.