Asiye kubali kushindwa si mshindani

asiyekubali kushindwa
asiyekubali kushindwa

‘Twende SOKONI LEO.’, Rasto Paka kamwambia Boflo panya.

‘Kuna nini kizuri sokoni ? ’ ,Boflo akauliza.

‘Mbuzi anauza mechi mzuri.’, Rasto akaeleza.

‘Mechi kuuzwa? Sielewi. ’, Boflo akasema.

‘ Wewe ni mshabiki wa mchezo wa kandanda ?’ , Rasto akauliza.

‘Mshabiki nambari mmoja’ , Boflo akajibu kwa kishindo.

‘Hebu fikiria kama ungeweza kubashiri michezo yote. Si hiyo ni utajiri?’, Rasto akaendelea.

‘Kweli kabisa nitakuwa kama nabii Owuor. Nitapata heshima kutoka mafans kwani watakuja kwangu kupata tafsiri.’, Boflo akasema akiwa anatafakari.

‘Hivyo ndivyo tunataka kufanya. Ukinunua mechi utakuwa unajua timu itakayo shinda hata kabla ya mechi kuanza.’,Rasto akasema.

‘Wenzangu watawacha kunichapa kila wakati timu yangu inaposhindwa.’, Boflo akaongeza.

‘Tukishajua atakaye kuwa mshindi tunaweza kuweka hela kidogo ili tupate kitu kubwa zaidi.’ , Rasto akaendelea.

‘Si huo ni mchezo wa kamari? ‘, Boflo akauliza.

‘ Kamari ni uwekezaji wa pesa tukibashiri ni timu ipi itakayoshinda. Tofauti kubwa hapa ni kwamba sisi tutakuwa tukishinda kila wakati si kubahatisha na kupoteza.’ ,Rasto akasema.

‘Sasa mimi ndiye nitakuwa nikiwachapa wengine. Kama huu mchezo sio kamari basi hii ndio kamari feki. Si hapo tutakuwa tukidanganya?’, Boflo akauliza.

‘Wachana na wengine haja yetu kubwa ni PESA.’, Rasto kamweleza Boflo.

‘Tutakuwa matajiri.’, Boflo akawaza. ‘ Lakini Mbuzi alipata nguvu zake za kubashiri wapi?’, Boflo akauliza.

‘Wasiwasi ya nini Boflo, mbuzi anatuuzia ukweli. Huwezi kupotezwa na ukweli!’, Rasto akaendelea.

‘Utamu wa mechi utaisha na aina hii ya ukweli. Hule msisimko hautakuwepo kwa vile tutakuwa tukijua matokeo wachezaji wakiwa uwanjani.’, Boflo akarudisha.

‘Maisha siku hizi imekuwa ghali hata ukweli inauzwa sokoni. Nitapika mboga bila nyama leo.’, Teke punda akasema.

‘Wamaanisha nini punda?’, Rasto akauliza.

‘Paka aanze kula mboga kama wale wengine.’, Teke akaendelea.

‘Unasema Paka ale mboga. Ndotoo ya ajabu hioo.’, Boflo akasema akiwa anatingisa kichwa chake.

‘Hujasikia kuna papa ambaye anakula mboga?’ , Tekepunda akawaambia.

‘Papa mla mamba na kiboko sasa anakula mboga? ’, Boflo akauliza.

‘Ndiyo. Papa huyu ambaye anamazoea ya kula nyama kusudi apate proteni anapenda kula mboga pia. Niko na Imani kuwa Rasto anaweza kubadilisha njia zake.’ , Tekepunda akaendelea.

‘Wewe humjui Paka.’, Boflo akamwambia Tekepunda. ‘Naweza kubali jua kubadilika kawa mwezi lakini Paka kula mboga haiwezekani.’ , Boflo akaendelea huku Paka akilamba lamba miguu yake.

‘Hofu ni ya nini Boflo?’, Tekepunda akauliza.

‘Naogopa Paka akikosa nyama leo atanitazama kama kileo.’ Boflo akalia.

‘Wewe huoni uchafuzi wa mazingira unazidi?’ Tekepunda akasema ,’ Na umechangiwa zaidi na ulaji wa nyama.’ akaendelea kusema.

‘Boflo, Boflo, umekwenda wapi?’, Tekepunda akauliza.

‘Rasto Paka uko wapi?’