Tunda jema halikawii mtini

tunda jema
tunda jema

‘Hii ni Kizungumkuti,  Rastopaka anashughuli gani na mende? ’, tekepunda akauliza.

Tekepunda na Boflo panya walikuwa jikoni. Walikuwa wakiosha vyombo baada ya kula.

‘Mende hakuna hapa jikoni. Wamehama?’, Tekepunda akauliza.

‘Huna habari? Paka amekuwa akifanya biashara ya mende.’, Boflo akaeleza.

‘Biashara na mende? Sielewi ,kwani Paka kabadilisha DIET?’, tekepunda akauliza kwa mshangao.

‘Binadamu ndo amebadilisha diet. Anasema kuwa hawa wadudu wana ladha nzuri.’,Panya akajibu.

‘Kwa hivyo hatakula nyama tena?’, tekepunda akauliza.

‘Binadamu haja wacha kula nyama bali ameongeza wadudu kwa chakula chake.’, boflo akaendelea na maelezo.

‘Tumechangia pia, haifai paka afaidike peke yake.’, tekepunda akasema.

‘Maarifa yake.’, Panya akasema.

‘Haifai jiko libaki bila wadudu.’, teke punda akasema.

‘Shida iko wapi Teke punda? Rastopaka ametuondolea hao wadudu. Haijalishi ni mbinu gani ametumia.’, Panya akateta.

‘Wewe unasema hivyo kwa sababu amekuondoa kutoka kwa menyu yake.’ , Teke punda akasema.

‘Hata hivyo ni ukweli kwamba paka amefanya kazi nzuri. Ukumbuke pia Paka ni mjanja.’, akasisitiza Panya.

‘Hakuna mdudu hata mmoja.Hii ni miujiza kweli.’, Teke punda akasema.

‘Shida zangu zimepungua sasa.’, boflo akasema.

‘Hali hii si nzuri kwa vile itatubidi tuwe tunakula bila kubakisha.’,tekepunda akaendelea.

‘Bora umalize kile umepika.’, Panya akamweleza tekepunda.

‘Hata viwavi paka amebeba…ni makosa.’, tekepunda akasema.

‘Masomo mingi ya nini punda. Kubali vile mambo yalivyo sasa . Isitoshe hali ya anga itabadilika.’,boflo akasema.

‘Hali ya anga hapa jikoni haijabadilika. Hewa ni ile ile.’, tekepunda akamalizia akiondoka.