Deni ya Galaxy Fold

kapewa kiti
kapewa kiti

Urithi wa mamilioni ya dola na dadake Paka anayeishi Marekani umewafanya wanyama wafikirie kwa kina kuhusu uhusiano wao na Binadamu. Dadake Paka ambaye anatambulika kwa majina Choupette alikuwa rafiki mpenzi wa binadamu Karl Lagerfeld tajiri mchoraji wa mavazi.

Hapo awali Karl alipoulizwa hatima ya paka wake mpenzi alijibu kuwa Choupette ataendelea kuishi kama kawaida na kwamba atashughulikiwa vyema hata baada ya kuondoka kwake. Alipoulizwa kuhusu urithi wa mali yake akasema iko mali ya kutembea kwa hivyo hakuna yule atakayekosa.

Akizungumza akiwa uwanja wa ndege Rasto paka alisema uhusiano kati yake na dadake ulikuwa kama chanda na pete. ‘Uhusiano ule unadhihirisha umuhimu wa kuwa rafiki wa binadamu.’, paka akasema. Hata hivyo kulikuwa na manu‘nguniko kati ya baadhi ya wanyama ambao walikasirishwa na matamshi yake.

Siku ya Ijumaa wanyama walimvamia paka wakitaka kulipwa deni. Baadaye paka aliwaambia kuwa atalipa maradufu kile walichokuwa wakidai. Wanyama walifurahi sana. Paka aliwaahidi kutoa hela walizodai kuanzia wiki ijayo atakapo kamilisha ziara yake huko Marekani.

Hii si mara ya kwanza kwa Rasto paka kukwepa kulipa wanyama wenzake. Punda alikuwa ameazima paka simu aina ya Galaxy Fold ili ampigie mama yake ambaye alikuwa hospitali. Punda akitokwa machozi akaeleza vile paka baada ya kuongea na mamake akaanza gumzo na wenzake na mwishowe kupotelea gizani. Hakuonekana tena hiyo siku na hatima ya simu yake haikujulikana.

Galaxy fold ni simu ya kifahari. Simu yenyewe ni nzito na matumizi yake pia ni mazito. Punda aliathirika sana kutokana na ulaghai wa paka.