Asifuye mvua imemnyea

mvua zima moto
mvua zima moto

Uzito wa kofi ulisababisha meza iliokuwa imepakana na jiko kuanguka na chakula kumwagika. Moto ukaanza hapo na kusambaa ndani ya msitu. Wanyama walitoroka mguu niponye. Miti na mito iliathirika kutokana na makali ya moto. Simba aliyekuwepo akiwa ametulia kabla ya kufikiwa na moto alitoroshwa pia.

Mzee Kobe akisimulia namna moto ulivvyo anzia ,’mara tu baada ya maombi nyati akamzaba fisi kofi akiwa amenyoosha mkono wake mezani akitaka kufikia sufuria ya nyama.’ Kunguru alikasirishwa na kitendo hicho na kusema kuwa kiongozi wa maombi ndiye mwenye mamlaka ya juu katika suala hilo.

Binadamu alipokuwa ziarani alimuokoa aliyedhani ni mbwa aliyetaabika baada ya kukwama chini ya kiti akitoroka moto. Hakufahamu kuwa alikuwa anamuokoa mbwa mwitu tofauti na mbwa mwaminifu.Binadamu alimpeleka mbwa mwitu hadi kituo cha kudungwa sindano.

Shambulio linalodaiwa kufanywa mle ndani linatajwa kuwaua viini hatari kutoka India. Hata hivyo msimamizi wa chumba cha sindano, Pakistan ,amekanusha madai kuwa India ingesambaa kwa vile hakuwa mbwa mwaminifu.

Changamoto kubwa atakumbana nayo Pakistan pindi atakaposhambuliwa na huyu mbwa, atalazimika kuamua kumkamata au kumuachia atoroke bila pingamizi.

Baadaye mvua ya masika ilinyesha na kuzima moto uliokuwa ndani ya msitu. Wanyama wa pori wanaendelea kukadiria hasara kubwa kufuatia moto uliozuka na kuharibu miti na rasilmali katikati ya msitu.

Akizungumza na kasuku , nyani alihofia maisha yake na kuwa halikuwa tukio la kawaida msitu kuteketezwa.

Mwenyekiti wa shirika la wanyama pori, Twiga mrefu, alisema kilichosababisha moto huo bado hakijajulikana na hamna aliye jeruhiwa vibaya wakati wa mkasa huo. Wanyama wengine walipinga ripoti kwa sababu twiga mrefu hana uwezo wa kufika MASHINANI.