Wadudu wafanya maandamano sababu kukosa umati

kunguni walia
kunguni walia

Wadudu kunguni waliokuwa wamejificha ndani ya viti walitoka mafichoni. Hali ambayo si kawaida. Mmoja wao, mdudu kunguni mmoja mkubwa alitikisa kichwa chake akitembea tembea kwenye viti vya basi. Hakuamini ile hatua umati wa binadamu amechukua ya kukaa nyumbani.

Hata salamu amebadilisha

Akiongea kwa sauti ya juu akasema, ‘ Sijaamini kuwa binadamu anaweza kuishi hivi. Hata salamu amebadilisha.’ Kunguni wengine wengi wakamjibu ,’ Turuke juu ya viti. Pengine binadamu atarudi akiona tukijiburudisha juu ya viti vyao.’ Mwishowe walichoka kwani hakuna umati wa watu ulioonekana ndani ya basi.

Pombe na sigara wamepiga marufuku.

Kisha mmoja wao akikunja uso wa hasira, akiwa nje ya mlango wa basi na akaanza kupiga kelele akisema,’Haki yetu. Haki yetu!’. Wale waliokuwa hai wakamuunga kwa kupiga kelele pia. Wengine walingongana na kuanguka chini.

Wakisomewa taarifa na nzi wenzao wakaambiwa,’ Binadamu amejifungia ndani ya nyumba na kukosa kwenda kazini. Isitoshe sasa hatuwezi kuingia ndani ya mdomo wake kwa kuwa ameziba na maski ya barakoa. Hapo awali alikuwa na mazoea ya kuingiza vidole vyake ndani ya pua.’

Hatuwezi kuingia mdomo wake kwa sababu ya maski.

‘Kila kona sasa kuna mtungi wa maji na sabuni wa kusafisha mikono. Hali hii imesababisha upungufu wa vijidudu ambavyo vimekuwa vikitusaidia kusambaza kinyesi.’ , nzi mkubwa akasema.

Binadamu anasema ataangamiza Malaria na maradhi mengine kabisa

Nzi mkubwa

Wazo 10

  1. Umenikumbusha utoto wangu! Kuna mtoto mmoja alinyimwa mkate na kumgeukia rafiki yake ambaye alikuwa tumbili.

Maoni yamesimamishwa.