HATUA ya mbwa na kiatu kufunga goli

mbwa hodari
mbwa hodari

Hakuelewa jinsi gani watu wanakimbizana na kung’ang’nia ngozi na hatimaye kutoa hadi machozi kwa furaha na wengine kwa machungu. Hili ndilo kitendawili kilichokuwa bila jibu kwake yeye mbwa.

Jambo hili lilimshangaza sana. Ndiposa akaamua kwanza avae sare kama wao ili aone kama atapata msisimko akibadilika. Akajiandaa vilivyo kwa kuhakikisha amesoma kila jambo kuhusu shughuli zinazotendeka uwanjani.

Kwa upande mwingine aliona wengine wakipiga makelele na kuimba. Lakini macho yote yalikuwa uwanjani yakitazama kidude kimoja kilichokuwa kikitoka upande mmoja hadi mwingine.

Pengine kuna utamu unaopata kwa kuiga wengine mbwa akawaza. Muhimu zaidi aliona ni kifaa kicho kuwa kikitumiwa kufukuza au kufukuzwa. Kifaa hicho kilikuwa kinajulikana kama kiatu.

Mmoja kati ya wale waliokuwa wakifukuzana akavua kiatu chake na mbwa kwa bahati yake akanyakua kile kiatu na kukimbia nacho. Kusema kweli macho yote yalimwangazia sasa hadi wengine wakaanza kumkimbiza. Kwa muda mchezo ulibadilika.

Mbwa alifurahishwa sana kukimbizwa na alipokamatwa alipongezwa na kupewa mnofu jambo ambalo hakuwa ametarajia. Kiatu kilibebwa na mguu tofauti na kuondoka mbio.

Mbwa alipojaribu kuingia uwanjani akazuiliwa. Baadaye akapelekwa kutazama kondoo malishoni.

Wazo 1

  1. Jambo msanii
    Sasa wewe msanii unaweza kusaidia kwa kuwa mjanja zaidi. Ulikuwa na jukumu la kuendesha blogi kwa ustadi na makini. Na mara nyingi unatoa chapisho ambayo inasaidia.

    Uliandika hivi karibuni kwamba mbuzi ni polisi. Jeshi pale DC haihifadhi pesa kwa sababu inagharimu zaidi ya mfumo wa sasa. Unapiga marufuku gharama za mfumo huu kwa urahisi kwa wanyama ambao hawawezi kufanya kazi kwa sababu ya maswala ya kiafya ambayo yangeweza kutatuliwa ikiwa yangeshughulikiwa mapema.

    Au mbwa wote walioathiriwa na kuzuiliwa kutoka Tanzania na mama ambao maisha yao wamehudumia ofisini. Hata hivyo kuzimwa kwa mtandao haukuleta uchaguzi Uganda. Kama sisi wadau wa sekta tumekuwa tukifanya kwa muda mrefu na tukasababisha Lil Wayne pamoja na sera nzuri.

    mchungaji magaa

Maoni yamesimamishwa.