VIONGOZI wa uchumi saba kuhama kwa roketi

nyangumi ndani ya taka
nyangumi ndani ya taka

“Lazima nile vizuri, siwezi kula vyakula vivi hivi tu,” akasema nyangumi baada ya kumtema binadamu ufuo wa bahari.

Binadamu alikuwa anadhani amepata makao mapya baada ya kuhama kutoka mawe moto yaliyokuwa yakitoka kwenye volkano.

Nyangumi alizama chini ya bahari na kuanza safari akiwa na hamu sana ya kula chakula. Alipofika katikati ya bahari akaona mashua na watu ndani yake. Macho yake yakawa makubwa na mdomo ukaanza kudodonkwa na mate. Sio kila siku anapata nafasi ya kuchagua kile alichokuwa akitaka. Baada ya kuzunguka ile mashua mara kadhaa, akasabibisha mawimbi makali yaliyomwaga maji ndani ya mashua ili izame. Waliokuwa ndani wakilia wasiangamizwe.

“Nataka dawa!”, akasema nyangumi.

Sisi ni wale viongozi wa uchumi saba na tuko kwa mkutano.”, wakajibu waliokuwa ndani ya mashua.

“Tuko hapa na suluhu kama unataka bitcoin”, wakaendelea kusema.

Nyangumi akafungua mdomo wake na wale viongozi wa uchumi saba wakapigwa butwaa.

Ndani mlikuwa mmejaa mikebe, sahani na vijiko vya plastiki.

‘Ulishindwa kumeza hii mikebe, sahani na vijiko vya plastiki?’, akauliza kiongozi mmoja.

Baadaye akazabwa kofi na kiongozi mwenzake.

Kiongozi wa tatu akatikisa kichwa, ‘Nilidhani kuwa tutapata mazingira rafiki baharini. Kumbe nilikosea.”

“Sasa kama hakuna la kufanya kwa nini mmejiweka katikati ya bahari?”, akauliza nyangumi.

“Tumepotea na hatuna suluhu kwa matatizo yanayoikabili dunia yetu.”, wakajibu wale viongozi wa uchumi saba.

Nyangumi akawaza na kuwaambia, ” Nitawaonyesha njia ya kuenda mazingira rafiki lakini nitahitaji mchunguze mdomo wangu ili mmweze kupata tiba yake.”

Wale viongozi wa uchumi saba wakajadiliana na kukubali kuingia ndani ya mdomo ya nyangumi. Hata hivyo viongozi wengine hawakuingia mdomoni bali waliwahakikishia walioingia mdomo wa nyangumi kwamba watawaunga mkono kwa dhati katika suala la usalama wao.

Viongozi hao wakazungumzia hatua zaidi za kuimarisha usafi wa mdomo,meno na ulimi ikiwemo kufanya kazi pamoja kupitia maji safi ya bahari kushughulikia changamoto zinazosababishwa na vyombo vya plastiki.

Hata hivyo wengine waliona sababu ya kuhama kwa roketi kutafuta mazingira bora.

Wazo 4

  1. Hatua ya kwanza katika kuanzisha uhusiano bora kati ya paka na mbwa ni kuhakikisha kuwa yeyote ambaye tayari anakaa nyumbani au ni mwenyeji asitatizwe na mabadiliko.

    Ni vema kupanga mapema juu ya mahali ambapo matandiko mapya ya huyu mgeni awe ni paka au ni mbwa, pahala pa malisho , vyombo vya kuchezea, nk, wataishi, na anza kuwatambulisha polepole na kuziweka angalau wiki mmoja karibu na nyumbani kwa hivyo sio kila kitu kitabadilika kwa wakati mmoja – atakayekuja atakuwa na wakati wa kuzoea hali mpya nyumbani kabla ya mgeni paka kuwasili.

  2. Msanii mwenzangu,

    Mimi ni mwanabloga. Na kama mtunzi najua kwamba huwezi kuchapisha nakala za stima, na soketi ziwekwe wapi na mataa yatawekwa wapi, au hata paa iweje kabla ya kukubaliana juu ya mifugo wanaishi ndani ya nyumba. Bila kujua idadi ya mbuzi, unapoteza muda. Sasa rangi ya nyumba yetu haieleweki hadi sasa iweje tuongelee viti na vitanda na kuta. Tukubaliane kuhusu mikeka tu na mambo yote mengine yatafuata.

Maoni yamesimamishwa.