NGURUMO ya simba yapotea na mdomo wa binadamu

samaki mezani aongea
samaki mezani aongea

“Itakuwaje wanyama wakianza kuongea kama binadamu?”, paka akawaza.

“Tutaweza kujua mengi zaidi!”, punda akachanga.

“Kweli, tutajua siri zake zote na yeye atajua zetu.”, paka akamjibu.

Samaki amabye alivuliwa apatikana na mdomo wa binadamu.

“Huoni hata binadamu hawaongei lugha moja. Kila kabila iko na siri yake.”, punda akasema.

“Sasa niambie vile utakavyokula. Utahitaji usaidizi wa vyombo vya binadamu vya jikoni kulia. Isitoshe utawezaje kukamata uma, wewe na kwato zako?” , paka akaongeza akimcheka punda.

“Kwa mara ya kwanza nitapata kujua utamu wa minofu mnayokula.”, punda akajibu.

“Mimi sitabadili mdomo wangu nianze kula nyasi na majani”, akasema paka huku akilamba miguu yake.

Panya walimshangila simba aliyekuwa akilia kutokana na sauti yake kupotea baada ya kuwekewa mdomo wa bindamu. Hata hivyo panya walionekana kufurahia masaibu ya simba ambaye alikuwa hapo awali tisho kwa wote.

Simba aliondolewa madarakani.

Katika hotuba yake kwa ndege wengine kuhusu mwenendo wa mawingu ,mbuni, alisisitiza umuhimu wao kutotumia maneno kiholela holela na kuzingatia tahadhari zilizowekwa kukabiliana na matamshi tofauti za lugha.

Hatua zingine zilizowekwa na mbuni kuzuia kuenea kwa uvumi ni pamoja na:

 • Wahudumu wa bahari na maziwa wataendelea na huduma zao hadi saa tatu usiku kwa kipindi cha siku 60.
 • Mbuni aidha amepiga marufuku misemo yote ya kisiasa kwa siku 30.
 • Mipango ya maji safi imedhibitiwa kwa muda wa saa 72, na watakaoruhusiwa kuogelea majini ni 10. Amri hiyo pia inahusisha kutaga mayai.

Matamshi makali yamekuwa yakitumika angani, hali inayoashiriwa kuchangiwa na hewa chafu kuachiliwa bila kuzingatia masharti yaliyowekwa kukubaliana na mdomo wa binadamu.

Ili kuhakikisha amri hiyo inatekelezwa kiongozi mbuni ametoa amri waseme wanavyotaka ardhini bila kujali madaraka yao.

Wazo 2

 1. I say
  mtu wangu pole sana mimi nilikuwa na tatizo hadi nikasoma nikifikiri ni bahari la kupotelea ndani. Bado nakushukuru sana kwa michoro kuwa umeweza kunisisimua akili kidogo na sasa nitaangalia chapisho zingine kujua kama mwendo ni huo huo. Ushauri wangu utumie methali na misemo nyingi kama za kale.

 2. Safi sana, sasa naona faida za mitandao ya kijamii habari kama hii ungeiweka kwenye FB au gazeti la kimataifa mimi nisingeiona, lakini kupitia samaki nimeiona, hongera sana.

  Sasa, uwe una toa ushuhuda kwa mafans wako wa takajua kuwa mitandao ya kijamii na hasa blogi hii inasaidia sana kutuchangamsha. Ningependa sana kuwa hivo kila siku

  FARM ANIMAL BEHAVIOUR WELFARE & ETHICS

Maoni yamesimamishwa.