Sheria na masharti

 

 1. Kwa kutumia takajua.com unakubaliana na sheria na masharti haya, ambayo yanaanza kutumika mara tu unapoanza kuingia takajua.com. Endapo haukubaliani na yote tafadhali usiingie, usitumie au uchangie takajua.com.
 2. Takajua multimedia Developers wanaweza kubadilisha masharti haya wakati wowote kwa hiyo ziangalie mara kwa mara.Utumiaji wako wa takajua.com utachukuliwa kuwa umekubali masharti yaliyoongezwa au kubadilishwa.
 3. Michango iliyo katika lugha nyingine isipokuwa Kiswahili huenda ikaondolewa au ikakosa kuchapishwa.
 4. Michango/Maoni inayotumwa takajua.com mara mingi ni ya kutoka kwa umma. Isipokuwa pale imeelezwa vinginevyo maoni hayo si ya Takajua Multimedia Developers.
 5. Unashauriwa kuchukua tahadhari zote kulinda kompyuta yako isiambukizwe virusi.
 6. Michango lazima iwe ya kujenga na yenye nidhamu, isiwe na lengo baya au iliyotolewa kwa kusudi la kusababisha usumbufu.
 7. Ili kushiriki na kutoa mchango katika sehemu zilizochaguliwa katika takajua.com utahitajika kujisajili.
 8. Watumiaji wa rika zote na uwezo huenda wakaweza kushiriki au kuchangia takajua.com. Picha za uchi haziruhusiwi.
 9. Michango iliyo nje ya mada au yenye lengo la kudhuru hairuhusiwi. Mchango ambao umeshatumika au unaofanana sana mara nyingi hautaruhusiwa.
 10. Tafadhali usiwasilishe mchango wako kwa mara ya pili kwa zaidi ya mjadala mmoja.
 11. Matangazo au usambazaji wa barua taka maarufu ‘spam’ hairuhusiwi.
 12. Usiwasilishe  mchango wowote ulio kinyume na sheria kwa namna yoyote ile katika kuchangia takajua.com. Usisambaze kwa makusudi au kwa uzembe barua yenye virusi vya kompyuta.
 13. Takajua Multimedia Developers imechukua tahadhari kuhakiki yaliyomo takajua.com kuepusha makosa, virusi au kasoro, hata hivyo Takajua Multimedia Developers haisemi kila kitu kitafanya kazi bila shida yoyote.