Watetea ndizi na mgomba si wako

“Nilikupa ndiziĀ  ukakataa. Angalia sasa tuko kotini. Mbona hivi?”, Paka akamwuliza Kunguru. ‘Mimi nilikuwa naelekea sokoni ndiposa nikakuona ukibeba ndizi’. Kunguru akajibu. ‘Wewe umewahi kuona paka akila ndizi?’, Paka akauliza. ‘Kusema kweli sijawahi kouna hata paka mmoja akila ndizi.’, Kunguru akajibu. ‘Mbona waniwekelea mambo kama haya. Mambo ambayo hayaeleweki?’, Paka akauliza tena. ‘Mimi nilikuona ukichuma… Soma zaidi

Ushahidi ndizi mahakamani

Kunguru alishika Kitabu cha Ukweli na kuapa kwamba atasema ukweli peke yake na kwamba hataongeza maneno ya kupotosha au kuwadanganya wasikilizaji. Mzee Kobe alirudisha Kitabu cha Ukweli na kuanza kumhoji Kunguru. Kunguru alikuwa mmoja ya kati ya wale walioshuhudia ndizi ikiibiwa. ‘Kwanza jitambulishe. Utuambie majina yako kamili na kule unakoishi.’, Mzee Kobe akaanza. ‘Kwa majina… Soma zaidi