HODARI sungura na gita ya stima

rockstar sungura

Mwanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama ‘gita namba moja’ aliimba wimbo wake ‘uchungu tamu’ kwa ustadi mkubwa. Wimbo ‘uchungu tamu’ uliwatoa machozi wengi waliokuwa katika hio hafla. Baadaye akaita wenzake punda na mzee kobe jukwaani kucheza ngoma yake. Akiongea na wanahabari sungura alisema kuwa ‘Hiphop’ imetoa fursa nzuri kusema ya ulimwengu wa leo. Rais Magufuli… Soma zaidi

HASEMI hacheki ananiangalia tu

kifaru na ndege

Sungura alijihisi kama mshukiwa na kumweleza mwenzake mzee Kobe, ‘Yule kifaru ananitazama sana.’ ‘Wasiwasi ya nini sungura?’, Kobe akarudisha. ‘Hasemi lile analolitaka. Hacheki na hakuna lingine analofanya ni kuniangalia tu.’ , sungura akaendelea. Mzee Kobe akatikisa kichwa kama kutoamini maneno ya sungura. Sungura akajificha nyuma ya kiti na kusema, ‘Kobe tazama, nikijificha bado aniangalia.’ ‘Wasiwasi… Soma zaidi

NANI alikula matunda ya Sungura?

alikula matunda

Duru za kuaminika zinaarifu kuwa mnyama asiyetambulika vizuri kutokana na giza iliyokuwepo alikula na kuiba matunda. Kulingana na nyati ambaye alikuwa akilinda huo mti, tumbili alipofika hapo alimdanganya kuwa yeye anauza dawa za kuboresha afya. Nyati akamwelezea kwamba yeye ni mzima na hahitaji kuboreshwa afya. Hata hivyo tumbili alimsihi aonje kidogo ili apate kujua zaidi.… Soma zaidi