Tembo anatunga wimbo wa kileo

ndovu wamelewa

Nani ako na masikio kama yangu? Masikio inayoweza kusababisha bendera kupeperusha. Nani ako na pua kama yangu? Pua linaloweza kuninyunyizia maji. Nani ako na miguu kama yangu. Miguu ambayo yamenipeleka kila kona ya msitu. Nani ako na mdomo kama wangu? Mdomo unaoweza kusiaga na kumeza miba. Kunaye anaye fanana na mimi?

Ni Kipigo cha Mbwa Koko?

mti na matunda

‘Jangili au binadamu, nani kaja mbele ya mwingine?’ ,tekepunda akauliza ‘Nafikiri jangili ndiye aliyetangulia.’ , Boflo akajibu. ‘Halafu binadamu kafuata baadaye.’ Rasto akaongezea. ‘Kwanza kifaru aliona binadamu lakini tembo akaona jangili na mwishowe simba akaona mnofu.’ , tekepunda akaendelea. ‘Mzoga sasa.’ Akasema Boflo kwa huzuni. ‘Binadamu jangili ataita wenziwe.’ , Rasto akasema. ‘Ataita wenziwe namna… Soma zaidi