Maendeleo bora

Hakuna mnyama anayekaribia binadamu kimaumbile kama vile nyani. Nyani ako na vidole kama binadamu, ako na sura kama binadamu na vilevile  ako na hisia na tabia kama binadamu.

Hapo zamani za kale kulingana na utafiti wa kisayansi bindamu hakuwepo. Yaani alikuwa kama nyani hapo mwanzoni. Alikuwa anatembea bila, alikuwa akiishi kichakani na hakuwa na matamshi yanayoweza kutunga sentensi au lugha. Inasemekana ugumu au changamoto zilizomkabili zilimfanya abadilike hadi kufika hapa alipo.

Tofauti kubwa kati ya binadamu na wanyama wengine ni uwezo wake wa kufikiri au kubuni vitu tofauti tofauti jambo lililomwezesha kuishi katika mazingira yeyote ile.

Kuna wale ambao wamekubali kuwa mwanzo binadamu alikuwa sawa na nyani na kuna wale ambao wamekataa kata kata na kusema binadamu aliumbwa.

Hata hivyo ukimwangalia nyani utakubali kwamba ‘ nyani haoni kundule’.