Asifuye jua limemwangaza

samaki majini

‘BOLSONARO anataka kubaki na mkono mmoja tu.. wa kulia. Nadhani wakati analia aweze kujipanguza machozi.’, Rasto akajibu.

‘Duh! Hana haja na mkono huo mwingine. Kwani mkono wa kushoto ulimkosea vipi?’,Boflo akauliza.

‘Kwani nani huyu anayetaka kujikata mkono?’, Tekepunda akauliza.

‘Ni kiongozi wa aina fulani binadamu.’,Boflo akajibu.

‘Wawezaje kuukata mkono wako bila kufuja damu? Haiwezekani.’, Rasto akasema huku akitingisa kichwa chake.

‘ Pengine hataki mkono wake wa kushoto kunyemelea mkono wake wa kulia.’ ,Tekepunda akaeleza.

‘Ajenge kuta kama anataka kuzuia upatanishi kama vile Donald.’, Boflo akachanga.

‘Kumbafu wewe! utawekaje kuta kuzuia mkono mmoja kuona ule mwingine?’, Tekepunda akauliza.

‘Ndivyo Trump anataka kufanya ili kusiwe na pingamizi maendeleo.’,Rasto akajibu.

‘Hiyo si demokrasia. Demokrasia ni uwazi.’,Boflo akaongeza.