Heri kuliwa na simba kuliko kuliwa na fisi

kimbia kwa simba

‘AMINI USIAMINI kupe wataka kuangamiza chatu!’, Boflo akawika.

‘Nakwambia chatu hana mikono wala miguu.’, Rasto akasema akitazama makucha yake.

‘Sielewi , mnyama mkubwa chatu amalizwe na kupe, si angekimbia?, Tekepunda akauliza.

‘Akimbie aende wapi na hao kupe wamedandia yeye kama sisi kwa basi. Hakuna kubanduka’, Boflo akaendelea.

‘Kwani walikuwa kupe wangapi?’ , Tekepunda akauliza.

‘Walikuwa kama mia tano hivi.’, Boflo akajibu.

‘MIA TANO! ’ Tekepunda akasema kwa mshangao. ‘ Dodo do !, Idadi hiyo imezidi jamii moja. Namhurumia chatu.’, akaendelea Tekepunda huku akitikisa kichwa chake kwa hofu.

‘Sikiza, chatu alitatizwa na kupe hao kiasi kwamba alitaka kuangamia nao majini ili kupunguza maumivu. Alijitumbukiza majini wafe wote.’ , Boflo akasema. 

‘Rasto anacheka ilhali yeye ako na hao kupe shingoni. Nini kilifanyika, chatu alifaulu?’,Tekepunda akauliza.

‘Binadamu msamaria mwema alimwona na kumuokoa. Alikuwa hali mahututi. Kupe walikuwa wamemfyonza damu mingi kutoka mwili wake. Sasa hivi anapata matibabu.’, Boflo akamalizia.

‘Sasa tufanyeje?’, Tekepunda akauliza.

‘Kwa nini wauliza hivyo?’, Boflo akarudisha.

‘Rasto asitupe hao kupe , watatuangamiza pia!,’Tekepunda akajibu.