Nguruwe apandishwa cheo

Dili moto
Dili moto

‘Wenzangu nawaambieni sasa MAISHA ni MILELE!’, Tekepunda akawika akitingisa miguu yake kwa shangwe.

‘Wamaanisha nini punda?’, paka akauliza.

‘Sasa hivi kama ukona upungufu wa kiungo chochote mwilini utaweza kupata kutoka kwa nguruwe.’, punda akajibu kwa furaha.

‘Mimi, nipate kiungo kutoka kwa nguruwe?’, paka akarudisha.

‘ Sikiza, inasemekana kuwa nguruwe wana mafanikio katika upandikishaji wa viungo vya viumbe tofauti.’, Tekepunda akasoma. ‘ Si maoni yangu ni sayansi.’

‘ Doh! Atakuwa kama duka ya viungo hivi karibuni. Nguruwe sio wa kuliwa peke yake..’, Boflo akachanga mawazo yake.

‘Wazo mzuri sana. Wazo mzuri.’, Rasto akasema akitazama anga. ‘Naonelea tufanye urafiki na nguruwe mara moja mapema mapema kabla wengine kutangulia.’ Rasto akaongeza.

‘Mimi sielewi.’ , Tekepunda akasema ‘  Ah! Unahitaji kiungo fulani kutoka kwa nguruwe na hutaki kutuambia, Kweli?.’  Tekepunda akauliza.

‘Hapo awali ulikuwa umesema MAISHA ni MILELE. Mimi naunga mkono kauli yako hiyo. Wengi wataangamia wasipopata matibabu ya dharura. Hao wachache ambao tutapata tuwalipishe kitu kidogo ilmradi tulishe nguruwe vizuri.’ , Rasto akaeleza.

‘Sikuamini. Wewe haja yako kubwa ni kutengeneza pesa sio kuokoa wenzetu.’, Tekepunda akarudisha kwa hofu.

‘Tunalisha nguruwe chakula kizuri kitamu hakuna yeyote ambaye tutakuwa tukidhuru hapa.’ , Rasto akaeleza.

‘Ni DILI nzuri sana au kwa kimombo WIN WIN. Kila mmoja ni mshindi.’ , Rasto akaendelea huku Tekepunda akitingiza kichwa chake kama asiyeamini alichokuwa akisikia.

‘Hata kama hutakubali kama Fayulu , sisi twaendelea au sivyo Boflo?’, Rasto akauliza.

‘Inavyoonekana mteja wa kwanza kubadilishwa kiungo atakuwa Tekepunda.’, Boflo akasema.

‘Kwa nini wasema hivyo?’, Rasto akauliza kwa mshangao.

‘Bongo lake latakiwa lifanyiwe ukarabati.’ , Boflo akajibu.  

‘Hapo umenena.’, Rasto akasema.