Maneno matamu hayatoshi kumtoa nyoka pangoni

maneno matamu

‘Do!, Binadamu hatakuwa na starehe msalani tena!’, kasema Tekepunda.

‘Kwa nini wasema hivyo? ’, Boflo akauliza.

‘Binadamu alitaka kuangamiza nyoka akiwa ndani ya choo.’ , Tekepunda akarudisha.

‘Walikuwa wamekosana?’, Boflo akaendelea kuuliza.

‘Sijui lakini inasemekana njia ya nyoka huyo kutoka chooni ilizibwa wakati binadamu alipokuwa akijisaidia ndipo akamng’ata akihofia kudhuriwa. ’ Tekepunda akasema.

‘Kudhuriwa kivipi?.’ , Boflo akauliza tena.

‘Jameni Boflo, hilo ni swali la kuuliza? Binadamu yuko ndani ya choo!’, Rasto akaingilia ,’Naye nyoka alikuwa ndani ya shimo la choo. Hukumbuki Trump akitueleza kuhusu sisi kama shimo la choo.’, Rasto akaendelea.

‘Aaah, nakubali kuwa nyoka angekufa na kupoteza maisha yake. Hata mimi ningehofia maisha yangu kutokana na shambulizi hiyo.’, Boflo akakiri.

‘Shambulizi tena?’, Tekepunda akauliza.

‘Wewe hujui? Uvundo unaotokana na kinyesi cha Binadamu umepita wa samaki.’ , Boflo akarudisha.
‘Uvundo peke yake imetosha kukuangamiza.’, akaongeza Boflo.

‘Nyoka alikuwa anafanya nini mle ndani?’, Rasto akauliza.

‘Maji. Alikuwa anatafuta maji.’, Tekepunda akajibu.

 ‘Binadamu alifanya nini baada ya kung’atwa na nyoka?’,Rasto akauliza.

‘Binadamu alifungua njia mara moja huku akipiga mayowe!’, Tekepunda akaendelea Boflo akicheka.

‘Binadamu alikuwa amefanya kosa kubwa kumfungia nyoka na kutaka kumuangamiza kwa njia hiyo.’, Rasto akasema.

‘Heri kupigwa risasi.’ , Boflo akaongeza. Baada ya kukaa kimya kwa muda mfupi ,Tekepunda akauliza , ‘Sasa itakuwa aje?’.

‘Pengine awe akienda kichakani kama sisi kwani hakuna haja ya starehe mingi msalani.’ , Boflo akasema.

‘Binadamu akona maadui wengi na siri mingi. Si rahisi ajisaidie eneo lenye uwazi.’ , Rasto akasema.

‘Sisi hapa ni marafiki na hakuna uadui wala siri yoyote.’, Boflo akasema.

‘Hapo nakubaliana nawe.’, Tekepunda akasema.