MBINU 3 za kuwinda wakati wa kiangazi

kondoo mitini
kondoo mitini

Kwa nini ubadilishe mkono, kwa nini ubadilishe mguu, kwa nini ubadilishe mdomo na tumbo ni ile ile. Katika harakati ya kuwinda tumbo ndio linaongoza au ndivyo wengi walikuwa wakifikiria.Haya ndio baadhi ya maswali yaliyoulizwa kwa mwalimu chui na wanyama wa kuwinda wanyama.

Baada ya kuyapokea yale maswali chui akajibu,’ Kwanza mazoezi ya mwili na maandalizi ya mapema ni lazima. Katika kuhakikisha mafanikio ni vyema kila siku kuruka juu na kwenda chini kuongeza nguvu za kutimua mbio.’

“Utafiti uliofanywa na kuku msomi unaonyesha kuwa pamoja na mazoezi kusaidia kupunguza madhara kama kuanguka ovyo na kuishiwa na pumzi pia yanachangia uwezo katika utafunaji wa nyama kwa hivyo huhitaji usaidizi wa mamba.’

‘Kuna vitu unahitaji kuambiwa ili usiangamie na njaa. Hapa niko na mbinu tatu za kujiweka katika hali ya kuwinda.’, chui akaendelea.

Ujiweke tope ili usitambulike. Katika makosa unayoweza kuyafanya unapoanza kuwinda ni kupuuza tofauti zenu za kimitazamo, kiimani na misimamo mingine ndani ya kichaka. Nikiona punda sifai kufungua mdomo kwa furaha.

Pili ni kutengeneza mgawanyiko kati ya wanyama. Nafahamu wanyama wakiwa wengi ni vigumu kuwakabili. Mara nyngi utahitaji mmoja kati ya kundi la wanyama. Siri hapa ni kutambua mmoja kati ya wengi upesi na kwa makini na kutomwendea au kujitambulisha mapema anapoonesha dalili ya kuondoka. Kaa mbali na umpe uhuru wa kupumua, kutenda na kuenenda vile anavyopenda. Unapofanya hivyo unamfanya ajisikie salama kufikiri na kutenda vile anavyotaka.

Mara nyingi tunakosa fursa ya kuwafahamu wale wanyama tu kwa sababu tunaonesha mapema dalili za kumtamani kama kitoweo bila kumkamata. Tunakuwa wepesi kubuni ndoto, kushiba hewa na kushangaa tunapokimbiza yule mnyama bila kufikiria. Matokeo yake wanyama wanakwenda na kupotelea kwa sababu ya maandalizi mbovu.

Tatu na muhimu zaidi ni kuwa mstahimilivu katika hatua za mwanzo za mawindo. Ingia kwenye uwanja kama wingu ili usitambulike ili uepuke msimamo yako kueleweka kirahisi. Kwa mfano, ikiwa unatafuta mbuzi , huna sababu ya kuliweka hilo wazi mwanzoni mwa mawindo kwa kufungua mdomo au kuonyesha makucha na kusababisha mbuzi kutoroka. 

Wazo 2

  1. Hongera sana msanii wa takajua kwa burudani na nakala safi ya blogi hii mnautupatia, Hakika nyinyi ni wadau wa kweli katika maendeleo ya mtandao
    Natamani blogi zote zikaiga mfano huu

Maoni yamesimamishwa.