MAVUNO ya bure bila kupanda mbegu

tumbili atazama
tumbili atazama

Lakini ilikuwaje? Tumbili mwenye ndoto nyingi, alikuwa amepewa jukumu la kusimamia shamba la mzee kobe kushughulika na uwizi na machafuko yaliyoongozwa na kiongozi wa zamani wa sungura aliyekuwa mlafi kupindukia.

Tumbili aliingia kazini jioni akiwa na fimbo kama ilivyokuwa desturi yake.

Alikuwa mmoja ya wale waliokuwa katika orodha ya wakati huo ya washika wezi kama nyati mlevi na kifaru usingizi ambao waliharibu kazi kwa kuzembea , jambo ambalo lilfanya wafutwe kazi bila malipo.

Wanyama wengi walifurahia kuingia kwa tumbili shambani wakiamini amekuja kupigania masuala yao.

Hata hivyo ujana wa tumbili, kwa mujibu wa ripoti ukawa majonzi.

Mara baada ya kuingia kazini badala ya kutulia na kukaa chonjo alianza kupiga stori akiwa anaruka mitini na ndege, jambo alilolifanya kuwa moja ya vipaumbele vyake vikuu. Tabia hii ndio ilitangaza kuwepo kwake shambani.

Hakukumbuka tena kuchunguza makelele tofauti yaliyokuwa yakitoka shambani kutokana na sungura kuvuna matunda. Yeye aliendelea kupiga stori na kulipokucha alipata matunda hayapo.

Haikuwa rahisi kwa mzee kobe kuthibitisha taarifa za tumbili kutokana na matatizo ya mawasiliano. Hata hivyo alikana kufanya makosa yoyote.

Wazo 3

  1. Daima ni kuweza kushuhudia mtazamo mbadala, na ni jukumu la mashabik kupiga kelele ndani ya blogi kama hii kwenye mtandao tunapoona moja kwa sababu ya ukweli halisi.

    Sungura alipoteza matunda matamu na mizeituni, kwa hivyo inaeleweka kwa nini kulikuwa na hasira kwake; wengi walikula matunda naye; sio kama kwamba matunda hayo yalikuwa na kasoro.

    Tumbili alitupa matunda?

  2. For one, your story is a bit too fast (not unlike the rest of your other posts in the blog)- putting all monkeys into one pot, so I’ll just say that for this tortoise, I totally disagree with those who would offer an mangoes to those drunk buffaloes you refer to, and would expand the list to include all animals up and down the jungle trees who have shown themselves to be unapologetic and deceitful thieves who deserve to be treated to the full extent of the jungle law.

Maoni yamesimamishwa.