NDEGE walalamikia ukosefu wa miti ndani ya mji

ndege na mwavuli
ndege na mwavuli

Katika kikao kimoja jijini, ndege wote walitua katika jumba la kimataifa.

Mbuni shingo mrefu akiongozwa na tausi mrembo, walimkataa kasuku magazeti kwa madai ya kushiriki na binadamu kutengeza viti na meza kwa mitindo tofauti tofauti ya kuandaa vyakula mezani.

Walidai tabia ya kasuku kushindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa katika vikao, huenda ikawakosesha mahala pa kujenga viota vyao na kutokuwepo kwa matawi yoyote ya maendeleo inayotekelezwa katika jamii zao.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mvua kunyesha na kufanya wao kuloa maji.

Hoja ya mbuni shingo mrefu, iliungwa mkono na baadhi ya bata ,hata hivyo, kuku rafiki ya kasuku , walisimama na kuwataka wanao paa angani kusitisha uamuzi wao kwa vile unapingana na utaratibu.

Jogoo mwika asubuhi alisema wanaopaa angani walipaswa waitishe kikao maalumu cha kutokuwa na imani na kasuku pamoja na kumwekea mayai yake kumzuia kupeperusha vumbio.

Hata hivyo, ushauri wa mbuni shingo ndefu, uligonga mwamba baada ya baadhi ya bata kusimama na kuanza kuchambua hoja hiyo ikiwamo maagizo yaliyotolewa kwenye vikao vya rafiki wa bianadamu jambo walilodai ni dharau inayooneshwa kwao na hawako tayari kufanya naye kazi.

Wazo 1

Maoni yamesimamishwa.