Ajabu Kondoo kucheka kioo

‘Aliingia vipi ndani ya soko?’, punda masikio kubwa akauliza.

‘Wewe unashangazwa na vile chatu alivyoingia sokoni. Hebu jiulize vile alivyokagua bidhaa kabla ya kununua?’, panya mla mkate akachangia gumzo.

‘Nyinyi mmepitwa na wakati. Hamjasikia kuhusu soko ya mtandao?’, paka akawaeleza akipapasa masharubu yake.

‘Tueleze hiyo soko iko wapi.’, punda masikio kubwa akarudisha.

‘Namuunga mkono punda, kwanza wacha kupapasa masharubu.’, panya mpenda mkate akaongeza.

Paka akainua mkia wake na kuitazama kama kungojea jibu na kusema,’Huhitaji kuondoka mahali ulipo. Kazi yako ni kubonyeza tu.’

‘Tangu nizaliwe nimebonyeza mara mingi sana maishani mwangu na sijawahi kuingia ndani ya soko.’, punda mwenye masikio makubwa akasema.

‘Kutafuta bidhaa na huduma mtandaoni kunaweza kuokoa muda na jasho kwa kukuruhusu kupata bei bora bila kulazimika kufanya kazi yote ya mguu. Unaweza kutumia mtandao kupata wauzaji wapya, kutuma maombi ya kununua au kutafuta kwa bidhaa na huduma.’, paka akasema akiunyorosha mkia wake.

‘Hata hivyo chatu mwona mbali alilipia vipi bidhaa alizotaka?’, panya mpenda mkate akauliza.

‘Alibonyeza na bidhaa zake zikaingia ndani ya kikapu.’, paka akajibu.

‘Kikapu ni bure au unanua kabla kuingia ndani ya soko?’, punda mwenye masikio kubwa akauliza.

‘Ukipewa kikapu ndani ya soko uweke bidhaa zako, utakataa?’, ,paka akauliza.   

‘Kweli chatu mwona mbali alifaidika kwa vile hangeweza kubeba bidhaa alizohitaji.’,punda mwenye masikio kubwa akasema.

‘Chatu mwona mbali hana kibeti cha kuweka fedha. Alilipia bidhaa zake vipi au alitumia vitisho kukwepa kulipa chochote?’, panya mpenda mkate akauliza.

‘Chatu mwona mbali aliendelea kubonyeza na mwishowe bidhaa zilifikishwa pangoni mwake.’, paka akawajibu.

Hata hivyo chatu alionekana ndani ya soko na kubabaisha wanunuzi wengine.