Hapo zamani za kale mwewe walikuwa marafiki na kuku. Wote wawili walikuwa karibu sana hivi kwamba waliamua kujenga nyumba karibu na kila mwenzake. Mwewe alijenga kiota chake karibu na vichaka ambako kuku alikuwa akiishi na binadamu.
Siku moja, mwewe alimwona mmoja wa watoto wa kuku akicheza. Wakati huo watoto wa mwewe walikuwa wakilia kutokana na makali ya njaa. “Nitafanya huyu kifaranga kuwa chakula kwa watoto wangu,” mwewe aliamua na kuruka chini na kumchukua mmoja wa watoto wa kuku.
Kuku aliporudi, aliona kuwa mtoto wake mmoja hayupo. “Umeona mtoto wangu?” Akauliza mwewe huku akilia muda wote. Maskini kuku aliumia moyoni na kupiga makelele. “Umenidanganya mwewe, mbona ninaona mabaki ya miguu ya kifaranga?,” akasema kuku na kukimbia na watoto wake.
Baadaye binadamu alitoka mbio mbio na kumfukuza mwewe. Kutoka hiyo siku mwewe amekuwa adui wa kuku .Hata hivyo hakuacha kutafutia watoto wake vifaranga.