Wimbo wa Nyangumi wamtoa ndege machozi

Hapo zamani za kale ndege na nyangumi walipendana sana kama chanda na pete.

Ndege alipenda vile nyangumi alivyocheza na maji. Alipenda jinsi alivyokuwa akiogelea kwenye maji kwa ujuzi.

Nyangumi alipenda sana manyoya meupe ya ndege. Alipenda pia kumtazama akipaa angani.

Wote wawili walipenda kula samaki wadogo wadogo.

Katika majira ya jioni ndege na nyangumi walikutana kwenye ufuo wa bahari. Hapo walizungumza juu ya mwezi, mawimbi na meli za bahari.

Ndege alimuuliza nyangumi vitendawili na kumfanya nyangumi kucheka. Nyangumi aliimba nyimbo nzuri zilizomfanya ndege kulia.

“Siku moja, nitakupeleka kuona marafiki zangu katika bahari”, akasema nyangumi

“Utakutana na marafiki zangu kwenye ardhi” , ndege alisema.

Mambo yalikuwa shwari

“Njoo nami kwenye maji matulivu”, nyangumi akamwambia ndege siku moja.

“Ni pazuri sana na kuna samaki wengi wa kula.”

Ndege aliposikia hayo alifurahi “ninapenda kula samaki”,

“Nitakufuata popote kwa sababu ninakupenda lakini kwanza nifundishe jinsi ya kuwa kama nyangumi.”

“Nifuate.”, nyangumi akasema na kupiga mbizi ndani kabisa ya maji ya bahari.

“Sawa”, akajibu ndege na kumfuata ndani lakini hakuweza kupumua. Ikabidi arudi juu ya maji kupumua.

Ndege alipojaribu tena aliishiwa na pumzi.

“Sidhani ndege anaweza kuwa kama nyangumi.”, ndege akamwambia nyangumi.

“Ninapenda kutazama jua linapochomoza,” nyangumi alisema. ” Nitakufuata popote kwa sababu ninakupenda. Lakini kwanza, nifundishe jinsi ya kuwa kama ndege”

“Fanya hivi!” Alisema ndege. “Nifuate!”, na akapiga mabawa yake na kupaa angani.

“SAWA!” Akasema nyangumi. Akafunga macho yake na kupiga mapezi yake, kama ndege. Alipiga makofi, huku akiruka juu na chini. Maji yalimwagika kila mahali. “Ninapaa!” alicheka. “Mimi ni ndege!”

Lakini alipofungua macho yake, hakuwa akipaa angani. Bado alikuwa ndani ya maji.

Alijaribu tena na tena, lakini hakuweza kupaa angani.

“Sidhani nyangumi anaweza kuwa ndege,” nyangumi akamwambia ndege.

“Lakini ikiwa huwezi kupaa angani, na siwezi kuogelea, tunaweza kuishi wapi pamoja?” Aliuliza ndege.

“Tutakaa hapa – katika ufuo wa bahari!” Akasema nyangumi.

Lakini ndege huyo akatikisa kichwa kwa huzuni.

“Unapenda kuogelea kwenye bahari,” akasema. Hilo ndilo jambo unalopenda kufanya. Huwezi kuwa na furaha hapa.” Ndege akamjibu.

 

 

Nyangumi akatokwa na machozi.

“Nawe unapenda kuruka na kupaa angani,” alisema. “Hilo ndilo jambo unalopenda kufanya. Huwezi kuwa na furaha hapa pia.”

Na hivyo, kwa sababu ndege na nyangumi walipendana sana, waliagana.

 

Lakini hakuna aliyesahau mwingine. Kila mara nyangumi alipomwona ndege akiwa juu angani, alimfikiria ndege. Alimtakia furaha ya anga.

Na kila wakati ndege huyo alipomwona nyangumi akipiga mbizi ndani kabisa ya bahari, alifikiria nyangumi. Alimtakia mema ya bahari.

 

Baadaye maji ya bahari yalibadilika na kuwa chafu. Samaki waliangamia wengi na nyangumi walitoroka ufuo wa bahari.