Mbweha anamwalika rafiki yake

Niko nyumbani kwa rafiki yangu kula na kucheza. Lakini chakula sio kile ninachokula kila siku.

Kuku alishtuka alipopewa tu ‘kipande cha nyama ya mwenzake, mbaazi kadhaa na vipande vichache vya karoti’ alipokuwa akisubiri kuandaliwa chakula kwenye nyumba ya rafiki wa Mbweha.

‘Mbona kushangaa?’, Mbweha akauliza alipoona sura ya kuku kubadilika.

Kuku akaondoka mezani bila kumaliza chakula chake au kusaidia vyombo.