Hapo zamani za kale palikuwa na mti wa matunda matamu sana katika bustani. Mti huu ulikuwa umesifika sana kwa kuwa na matunda matamu zaidi kuliko yote.
Wakati moja katika msimu wa matunda kulikuwa na majadiliano. Matunda walikuwa wakishauriana na kupeana moyo kwa sababu wataliwa au kupelekwa mbali na kuzaliwa kwao.
Mmoja wao alikuwa na kiburi kwa vile alikuwa ameiva sana. Utamu wake ulikuwa unavutia watu lakini alikuwa juu zaidi na hangeweza kufikiwa.
Wenzake walitolewa na kwenda mbali lakini yeye alibaki. Mwishowe kipepeo alitua juu yake na kutaga mayai yake. Baada ya siku kadhaa tunda lile tamu lilionekana na kiwavi akitokea kwa shimo moja.