Morani aliona chupa kubwa mezani. Alifurahishwa na bahati nzuri aliyoipata, akafungua kifuniko na kuweka mkono wake ndani ya chupa.
Morani alikamata biskuti nyingi kadiri mkono wake mdogo ungeweza kushika. Lakini alipojaribu kuutoa mkono wake kwenye chupa alishindwa kwani alikuwa ameshikilia biskuti nyingi sana!
Aligeuza mkono wake huku na kule, akijaribu kuutoa mkono wake bila kuwachilia zile biskuti, lakini hakufanikiwa.
Alidhamiria kupata yote. Hakulegeza mkono wake hata kidogo. Mama yake akamwita.
Nitafanyeje? Musa akajiuliza . Akakumbuka vile alivyoadhibiwa kwa kutosikia na mara moja akaachilia zile biskuti na kutoa mkono wake kutoka kwa chupa.