mpishi mbweha
“Nilidanganywa. Nilidanganywa, kama mjinga,” mbweha alinguruma, akitazama malisho tulivu kwa mbali.
Hakuna kondoo hata mmoja karibu anayeonekana.
Hakuna dalili ya mtu mmoja ambaye amekuwa akimngoja usiku kucha—Musa, mchungaji wa kondoo.
Yote yalianza wiki moja iliyopita wakati mbweha alipomsikia Musa akizungumza katika soko la kijiji. Alikuwa akitazama nyuma ya masanduku ya mboga, akijaribu kutafuta chakula rahisi alipomsikia mchungaji wa kondoo akisema jambo ambalo lilimvutia. “Nimepanga karamu kubwa wiki ijayo,” Musa alimwambia rafiki yake.
“Karamu karibu na maji mazuri wakati wa machweo ya jua. Lete njaa yako!” “Sikukuu?” aliwaza mbweha. “Safii!, nitaleta njaa yangu, sawa.”