Mechi ya ndovu

Kipenga kikapulizwa, mchezo ukaanza. Paka aliruka uwanjani, mwendo wake wa haraka na wa ucheshi. Punda, aliyedhamiria na mwenye nguvu, alipiga mpira kwa nguvu zake zote. Lakini ikawa wazi kwamba tembo alikuwa na nia tofauti la jinsi mchezo unapaswa kuchezwa. Kila wakati paka au punda alipofika karibu na mpira, tembo alikuwa akiruka kuelekea kwao, miguu yake … Endelea kusoma Mechi ya ndovu

Ushujaa wa mbuzi mwerevu

Katika kijiji kimoja kilichoko kati ya vilima, kuliishi mvulana mdogo aliyeitwa Soi. Soi alikuwa mtoto mwenye moyo mkunjufu na mdadisi ambaye alipenda kuchunguza malisho na misitu karibu na nyumba yake. Alikuwa mtoto wa pekee nyumbani alikoishi na nyanya wake katika jumba lililozungukwa na kijani kibichi na mbuzi mmoja mwerevu . Huyu mbuzi hakuwa mbuzi wa … Endelea kusoma Ushujaa wa mbuzi mwerevu

Supu moto yamtia flamingo woga wa maji

Samaki na flamingo walipenda sana kuogelea ziwani. Kwa sababu hii wakawa marafiki. Kila walipokutana katika ziwa majisafi flamingo alimpa samaki uhondo za kule alikokuwa na yale aliyoyaona. Samaki naye alimhadithia flamingo matukio ya kule ndani majini. Wakati mwingine flamingo alimhadithia samaki kuhusu vyakula vitamu alivyokuwa akila milimani na ndio sababu alikuwa na afya nzuri. Alisema … Endelea kusoma Supu moto yamtia flamingo woga wa maji

Garindege apotea njia baada ya kumtoroka ndege

“Mimi ni bora zaidi kuliko wewe,” Garindege akajionyesha kwa magari mengine. “Kweli wewe uko sawa” lile gari kuukuu jeupe likakubali. “Wewe ni mrembo na umeendelea kiteknolojia kuliko sisi wengine. Unaweza kupaa angani pia.” “Na nilisahau kukuambia kitu,” akasema Garindege. “Kioo changu cha kutazama nyuma pia huona kama jicho la kinyonga kama mfumo wa ufuatiliaji wa … Endelea kusoma Garindege apotea njia baada ya kumtoroka ndege

Wimbo wa Nyangumi wamtoa ndege machozi

Hapo zamani za kale ndege na nyangumi walipendana sana kama chanda na pete. Ndege alipenda vile nyangumi alivyocheza na maji. Alipenda jinsi alivyokuwa akiogelea kwenye maji kwa ujuzi. Nyangumi alipenda sana manyoya meupe ya ndege. Alipenda pia kumtazama akipaa angani. Wote wawili walipenda kula samaki wadogo wadogo. Katika majira ya jioni ndege na nyangumi walikutana … Endelea kusoma Wimbo wa Nyangumi wamtoa ndege machozi