Watu kuvutiwa na ngoma ya chui
Wanyama walitoka mbali ili wapate kusikia ngoma. Hadithi za porini zilisikika katika hiyo ngoma. Kila mnyama alishangaa kusikia habari na matukio ya porini na kufanya wao kufuata sauti yake. Ungedhani wanyama walikuwa wanatafuta chakula lakini ni utamu wa wimbo wake.