Tunda mtamu akataliwa kwa sababu ya kiwavi

Hapo zamani za kale palikuwa na mti wa matunda matamu sana katika bustani. Mti huu ulikuwa umesifika sana kwa kuwa na matunda matamu zaidi kuliko yote. Wakati moja katika msimu wa matunda kulikuwa na majadiliano. Matunda walikuwa wakishauriana na kupeana moyo kwa sababu wataliwa au kupelekwa mbali na kuzaliwa kwao. Mmoja wao alikuwa na kiburi… Soma zaidi »

Ndovu ana nguvu kiasi gani?

Ingawa wanyama wakubwa walizunguka hii dunia muda mrefu kabla ya wanadamu kuishi ndani yake, tembo ndio mnyama wa karibu zaidi ulimwengu wa zamani za kale. Ukiwalinganisha, tembo ni mdogo kuliko wenzao wa kabla ya historia. Lakini usipotoshwe kwani hawako karibu na viwango vya leo! Wanyama hawa ndio mamalia wakubwa zaidi wa ardhini. Kwa bahati nzuri… Soma zaidi »

Sungura apata chai ya mbweha

Habari zilienea kote kichakani kuhusu maisha ya kifahari ya sungura. Mbweha akapanga njama ya kuwa meza ya sungura ili aweze kuwekewa chai. ‘Habari gani hii?’, punda akauliza ng’ombe. ‘Nimeshangaa pia mimi. Yawezekanaje mbweha kuwa meza ya sungura?’, ng’ombe akauliza. ‘Najua sababu. ‘ , punda akajibu. ‘Mbweha kama meza ako na miguu minne.’, punda akaendelea. ,Wewe… Soma zaidi »

Ngamia asakata rumba uwanjani

Wengine walihema na kuangamia uwanjani kutokana na ukosefu wa maji na joto kali. Ngamia walionekana kama kuwa na miili yenye kuzuia makali ya jua. Mabao yalifungwa mengi huku wapinzani wao wakilalamika mazingira ya mchanga na upepo mkali. Ngamia wamekuwa kwenye fomu nzuri zaidi msimu huu. Wakiwa hawajapoteza hata gemu moja mfululizo katika gemu zao .

Supu moto yamtia flamingo woga wa maji

Samaki na flamingo walipenda sana kuogelea ziwani. Kwa sababu hii wakawa marafiki. Kila walipokutana katika ziwa majisafi flamingo alimpa samaki uhondo za kule alikokuwa na yale aliyoyaona. Samaki naye alimhadithia flamingo matukio ya kule ndani majini. Wakati mwingine flamingo alimhadithia samaki kuhusu vyakula vitamu alivyokuwa akila milimani na ndio sababu alikuwa na afya nzuri. Alisema… Soma zaidi »

Watu kuvutiwa na ngoma ya chui

Wanyama walitoka mbali ili wapate kusikia ngoma. Hadithi za porini zilisikika katika hiyo ngoma. Kila mnyama alishangaa kusikia habari na matukio ya porini na kufanya wao kufuata sauti yake. Ungedhani wanyama walikuwa wanatafuta chakula lakini ni utamu wa wimbo wake.