Garindege apotea njia baada ya kumtoroka ndege

“Mimi ni bora zaidi kuliko wewe,” Garindege akajionyesha kwa magari mengine.

“Kweli wewe uko sawa” lile gari kuukuu jeupe likakubali. “Wewe ni mrembo na umeendelea kiteknolojia kuliko sisi wengine. Unaweza kupaa angani pia.”

“Na nilisahau kukuambia kitu,” akasema Garindege. “Kioo changu cha kutazama nyuma pia huona kama jicho la kinyonga kama mfumo wa ufuatiliaji wa kielektroniki. Ninaporudi nyuma, inanionyesha kama kuna gari au kitu nyuma yangu. Hutoa sauti kunitahadharisha ikiwa iko karibu sana nami.”

“Unajua kule hakuna kurudi nyuma?” akauliza gari nyeupe.

“Ndiyo, niko na mataa na breki ” lile Garindege akajibu kwa kujigamba.

Mara tu, Domowazi, ndege akapita. Kila siku, alikuwa na mazoea ya kupanda juu ya tumbo ya gari nyeupe na kuwacha kinyesi chake. Leo, pia alipanda gari nyeupe. Lakini akamwona Garindege na kuwaza, “Hili hapa gari ni ya kifahari. Leo nitapumzika juu yake.”

Garindege aliingiwa na hofu kuona Domowazi akijiandaa kuruka juu yake. “Ikiwa ndege huyo atanikalia tumbo, atasababisha hasara. Ni lazima nimkwepe,” liliwaza lile garindege.

Domowazi aliporuka, Garindege akamwondokea haraka na kumshangaza. Domowazi akaanguka chini tifu. Aliumia. Alinyanyuka na kumkemea Garindege kisha akaondoka zake.

Baada ya muda Garindege akasema, “Naenda safari ya angani “.

“Utajua kule angani hakuna barabara au mataa za trafiki.” ,akasema gari nyeupe.

Hapo hapo, Garindege akajibu. “Nikifika kule angani nitajua la kufanya”.