Mkate chungu ni ya chungu

Katika nyumba moja, kulikuwa na mvulana aliyekuwa anaitwa Mwachofi. Mwachofi alikuwa mtoto mcheshi sana, lakini alikuwa na tatizo— miguu yake yalikuwa na uvundo.

Mwachofi alipenda kutembea bila viatu, hata katika sehemu ambazo mtu hangethubutu kukanyaga. Alikuwa akitembea kwenye madimbwi yenye matope, akitembea juu ya takataka, na kukanyaga-kanyaga na kutifua vumbi, yote bila kujali hali yake ya afya.

Baada ya muda, miguu yake ilichafuka na kunuka hata marafiki zake walianza kumkwepa.Lakini kulikuwa na mdudu mmoja ambaye alivutiwa na miguu yake Mwachofi. Kwa kweli, alionekana kumpenda sana. Mdudu huyu alikuwa chungu mdogo aliyeitwa Tito.

Tito aliishi na jamaa zake kwenye ufa kwenye ukuta karibu na nyumba. Tofauti na mchwa wengi, Tito alikuwa ana hisi ladha ya kipekee ya harufu isiyo ya kawaida kutokana na miguu ya Mwachofi.
Kila siku, Tito alikuwa akifuata mkondo wa uvundo, akiinuka kwa hamu na kupanda miguu ya Mwachofi kila alipoketi.

Hapo mwanzo, Mwachofi hakuwa anamwona yule chungu ,Tito. Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda,Tito alizidi kuwa jasiri. Wakati wowote Mwachofi alipokuwa akikaa kwenye kochi kutazama runinga au kulala chini ili kusoma kitabu, Tito alikuwa akinyata hadi miguuni mwake na kuanza kumtekenya kwa miguu yake midogo ya chungu.

Mwachofi alikuwa akiruka juu na kupepeta miguu yake,lakini Tito alikuwa mwepesi sana. Alikimbia, na kurudi  tu dakika chache baadaye.

Mchezo huu uliendelea kwa siku nyingi, hadi alasiri moja, Mwachofi alipoamua kupumzika kwenye meza tayari kula chakula. Akiwa amekaa akiwa amekunja miguu, Tito aliona nafasi yake. Akapanda juu ya kiti na kujiweka kwenye mguu wa Mwachofi, akimlamba lamba tena.

Mwachofi hakuweza kuvumilia tena. Alisimama kwenye kiti, na hatimaye, akaishia kukaa kwenye meza, huku miguu yake ikiwa imeinuliwa juu hewani ili kuepuka mateso ya Tito.

Akiwa amekata tamaa na kufadhaika, Mwachofi alimwita mama yake.”Mama! Kuna chungu huyu anayenitatiza na kunisumbua! Hataniacha peke yangu!”