Simba tisa watazama watalii

Simba walikuwa wamelala msituni, kila mmoja alikuwa amelala kifudifudi kutokana na makali ya njaa . Hapo karibu panya mdogo alipitia akiwa na woga na bila kutarajia na katika harakati ya kuondoka, alikimbia ndani ya pua ya Simba mmoja.

Akiwa ameamshwa kutoka usingizini, simba alimkamata panya kwa makucha yake makubwa kwa hasira .

“Nisamehe!” aliomba maskini Panya. “Naomba uniachilie na nitakuambia siri.”


Simba alichekeshwa sana na wazo kuwa Panya angeweza kuwasaidia. Panya alikuwa mdogo na maskini sana. Huyu simba aliwaamsha simba wengine na kuwaonyesha kile alichokuwa nacho kwa makucha.

“Umepata cha kula”, mmoja wa wale simba alisema.

Yule panya mdogo alifungua kinywa chake na kusema akiwa anatetemeka , “Nitawaambia kule mtapata minofu ya nyama.”

Yule simba aliye kuwa naye alimweka chini na wengine walimzunguka.

“Tuambie hiyo siri “, mmoja wa wale simba alisema.

“Nikiwaambia mtapata kula na kushiba.” , panya aliendela kusema.

“Tuambie upesi “, simba mwingine alitamka huku akidondonkwa na mate.

“Kuna mbwa mmoja ambaye anachunga boma ya mbuzi kumi.”, panya alisema.

Simba walijadiliana na kukubali kwenda kuona boma ya mbwa wa mbuzi kumi.

Simba hawakuwa wamekula kwa siku nyingi na walikuwa wanahofia kufa kwa njaa. Waliamua kwenda kwa boma ya mbuzi kumi usiku.

“Tukiambulia patupu tutakumeza kwa kutudanganya.’, simba walitisha yule panya.

“Tahadhari sana, binadamu wanaishi kule.”, aliwaonya panya.

Simba walipuuza maneno ya panya na kuingia katika ile boma. Mbwa alianza kubweka. Simba walimwambia mbwa awache kupiga makelele. Kwa hili, mbwa aliraruliwa matumbo na kupoteza maisha yake.

Simba walipata mbuzi wakiwa wamelala na bila kusita waliwashambulia na kula wote kumi.

Binadamu alipoamka alipata mbwa wake bila matumbo na mizoga ya mbuzi wake kumi . Kwa huzuni alilia kwa sababu ya kifo cha mbwa na hasara ya kupoteza mbuzi wake.

Panya maskini aliposikia binadamu akilia aliingiwa na hofu na kumweleza kuwa simba tisa waliingia boma yake usiku wa manane.

Binadamu aliingiwa na hasira alipoambiwa kwamba simba tisa walivamia boma yake na kusababisha kifo cha mbwa wake na kula mbuzi kumi. Panya hakusita kumwambia maskani ya wale simba tisa.

Binadamu pamoja na wenzake walijihami na kwenda kule wale simba walikuwa mafichoni. Simba wote walikuwa wamelala chali kutokana na shibe ya kula mbuzi kumi.

Binadamu wa kwanza alipowaona alipiga mayowe na wengine wakawarukia na kuwaangamiza wote. Wale simba tisa hawakuweza kutoroka kwa vile walikuwa wameshiba.