HAKUNA saa linalomsubiri mfalme

bodaboda moto

Wote walikuwa barabarani wakiendesha pikipiki. Punda alikuwa na yake. Paka alikuwa na yake. Simba alikuwa na yake. Kifaru alikuwa na yake. Mbuni alikuwa na yake. Sungura alikuwa na yake. Fisi alikuwa na yake. Mbuzi hakubaki nyuma alikuwa na yake pia. Barabara ni moja. Shughuli ni tofauti. Nani atampisha mwingine?