Samaki akilia machozi yabaki baharini

Mzee Kasumba hakulala hiyo siku alipoambiwa atafute machozi ya samaki.

“Nitajua aje ni machozi? Nitajua kama ni maji?”, mzee Kasumba akaijiuliza.

Kukamata machozi ya samaki haikuwa rahisi , kwa sababu samaki walikuwa ndani ya maji kila wakati, pamoja na machozi yanahitaji kuhifadhiwa vizuri ikiwa yatapatikana. Mradi huu unahitaji subira sana.

Mzee Kasumba alijaribu mbinu nyingi kutega samaki na jinsi ya kuhifadhi machozi ipasavyo mara tu alipowakamata.

“Katika majaribio mengi nilinasa maji chumvi bila kujua. “

Siku moja mzee Kasumba alipata kuvua samaki wengi lakini hakupata hata tone moja la machozi.

“Mzee unatatizo gani?”, samaki mmoja akauliza.

Mzee Kasumba alikuwa akilia aligutuka na kushindwa kutamka.

“Usiwe na hofu niambie unachotaka”, samaki aliendelea kusema.

Mzee aliporudiwa na fahamu alijibu kuwa alikuwa akitafuta machozi ya samaki.

Samaki kusikia hayo alishangaa na kumuliza sababu ya kutaka machozi ya samaki.

Mzee Kasumba akamweleza kuwa angelipata utajiri ikiwa angelipata machozi yake.

“Nirudishe majini basi”, samaki akamjibu “Nitakueleza jinsi utakavyopata machozi yangu.” , samaki akaendelea.

Bila kufikiria mara mbili mzee Kasumba akatupa yule samaki majini na kusubiri jibu.

Muda uliyoyoma bila jibu na kwa hasira akatupa takataka ndani ya maji ili samaki arudi kutoka majini.

Hadi leo maji baharini imejaa takataka kwa sababu hakuna aliyewahi kuona machozi ya samaki.