KARIBU..

‘Mbona Dereva Mbuzi anaendesha basi kama mwenda wazimu?’, Tekepunda akauliza. Basi lilikuwa linaendeshwa kwa kasi sana. Tekepunda, Boflo na Rasto walikuwa wakihofia maisha zao.

‘Ni kama tumemkosea.’, Boflo akasema. ‘Sidhani ni hivyo.’, Rasto akawaambia.

‘Anatuendesha vibaya na sisi wanyama hatustahili kubebwa hivyo.’, Tekepunda akasema kwa hasira. ‘Eeei Mbuzi sio viazi unabeba. Tunakuomba ujali masilahi.’, Tekepunda akawika.

‘Je, umeona vile anapiga miayo mfululizo?’,Boflo akauliza. ‘Hajalala usiku ’,  Rasto akajibu.

‘Kwani nini kilifanyika?’ ,Tekepunda akauliza.

‘Huoni hata mimi leo mchovu. Jana si kulala vyema kutokana na vurugu iliyokuwa katika boma ya Mbuzi.’,Rasto akaeleza.

‘Sasa tufanyeje?’, Boflo akauliza.

‘Maombi sasa la sivyo tutaangamia hapa’, Tekepunda akasema.

‘Dereva simamisha gari!’,Boflo akawika. ‘Nini tena?’, Mbuzi akauliza.

‘Nataka kujisaidia.’,Boflo akajibu.