Ng’ombe wa Professa Mwalimu

ng'ombe na mwavuli
ng’ombe na mwavuli

“Ng’ombe wangu ananila majani kuliko faida ninayopata. Lazima nitafute njia kumuuza!”, akasema Professa Mwalimu.

‘Nitakuonyesha jinsi ya kuuza kisasa’, kijana moja kwa jina Farifari akamwambia.

Akamchukua Ng’ombe, akampiga picha kwa kamera ya simu ya “kabambe”, akapakia mtandaoni akitumia akaunti yake ya X (zamani Twitter) na kuandika:

🐄 “Ng’ombe mwenye akili,  Bei ni rafiki, DM kama uko serious!”

Lakini hakukata tamaa. Akatengeneza TikTok video:
Ng’ombe anayeimba wimbo wa taarab huku anatafuna majani. Ilivuma! 🎶


Kioja Kianzia Hapo…
Siku moja akapokea ujumbe:

“Naitwa Daudi kutoka Kitengela. Nimeona ng’ombe wako anaweza kuwa mgeni wangu maalum wa harusi!”

Professa Mwalimu akasema:

“Pesa kwanza, mdomo baadaye.”

Daudi akatuma M-Pesa, elfu sabini na tano.
Bila hata kuonana. Bila mikono kusalimiana. Bila mguu kuangalia kwato.
Ni mtandao tu na picha.


Lakini Subiri…!
Professa akatayarisha usafirishaji, akampeleka Ng’ombe hadi kituo cha matatu kwa pikipiki — lakini ng’ombe aligoma kupanda.
Akapiga kelele kama mtu:

“MOOO… sitaki kuuzwaa mtandaoniii!”

Watoto walicheka, watu walipiga picha. Ng’ombe akawa maarufu kuliko Professa.