Mchungaji kondoo achelewesha mbweha karamu

mchungaji kondoo na mbweha

“Nilidanganywa. Nilidanganywa, kama mjinga,” mbweha alinguruma, akitazama malisho tulivu kwa mbali. Hakuna kondoo hata mmoja karibu anayeonekana. Hakuna dalili ya mtu mmoja ambaye amekuwa akimngoja usiku kucha—Musa, mchungaji wa kondoo. Yote yalianza wiki moja iliyopita wakati mbweha alipomsikia Musa akizungumza…

Chui mgeni wa mbwa nyumbani

mtazamo wa chui mtini na mbwa

Usiku wa manane, baada ya wenyeji wa kijiji kulala na kuwa kimya na nyota na mwezi kujitokeza, Sanjit alisikia sauti ya ajabu ikivuma nje. Alijipenyeza kwenye dirisha lake na kuchungulia nje, akiwa na shauku ya kutaka kujua. Kwa mshangao wake,…

Mzee kobe aongoza njia kwenda nyumbani

Kazee na Wazibe

Katika kijiji cha Usembo uliokuwa kando na pori, aliishi kijana mmoja aliyeitwa Wazibe. Alijulikana kwa ujasiri wake na moyo uliojaa fadhili, lakini siku moja, alikumbwa na msiba ambao haukutarajiwa. Kulikuwa na kiangazi na fisi mmoja akitafuta chakula akapata mwanya katika…

Chungu ni chungu alia Mwachofi

mtoto analia mama

Katika nyumba moja, kulikuwa na mvulana aliyekuwa anaitwa Mwachofi. Mwachofi alikuwa mtoto mcheshi sana, lakini alikuwa na tatizo— miguu yake yalikuwa na uvundo. Mwachofi alipenda kutembea bila viatu, hata katika sehemu ambazo mtu hangethubutu kukanyaga. Alikuwa akitembea kwenye madimbwi yenye…

Tumbili papa na chui

tumbili juu ya papa

Hapo zamani za kale, tumbili mmoja mwerevu alijikuta mahali pabaya na chui mwenye njaa. Chui alikuwa amemfukuza hadi kwenye ufuo wa bahari , akiwa ametoa makucha makali kwa mawazo ya chakula kitamu. “Usinile!” aliomba tumbili, akitetemeka kwa hofu. “Sina ladha…

Fisi ajionea maajabu mjini

fisi mjini usiku

Katika msitu mmoja, uliokuwa na miti mengi aliishi fisi mvivu moja aliyekuwa anaitwa Huru. Tofauti na fisi wenzake ambao walikimbizana na kuwinda katika msitu, Huru mara nyingi aliota juu ya jiji la mbali alilosikia kutoka kwa ndege. Walizungumza juu ya…

Mechi ya ndovu

tembo kuamua mshindi

Kipenga kikapulizwa, mchezo ukaanza. Paka aliruka uwanjani, mwendo wake wa haraka na wa ucheshi. Punda, aliyedhamiria na mwenye nguvu, alipiga mpira kwa nguvu zake zote. Lakini ikawa wazi kwamba tembo alikuwa na nia tofauti la jinsi mchezo unapaswa kuchezwa. Kila…

Kiboko akatalia ndani ya mto

mvuvi na kiboko

Mzee Jengo alipigwa butwaa kuona mnyama mkubwa ajabu mtoni. Hakudhania inawezekana kupata mnyama mkubwa kuliko ng’ombe wake chini ya maji. Joto iliongezeka na idadi ya samaki katika mto huo ulikuwa umeanza kupungua. Wanakijiji, wakiwa na hamu ya kulisha familia zao,…

Ushujaa wa mbuzi mwerevu

watoroka mbuzi hawana uhakika

Katika kijiji kimoja kilichoko kati ya vilima, kuliishi mvulana mdogo aliyeitwa Soi. Soi alikuwa mtoto mwenye moyo mkunjufu na mdadisi ambaye alipenda kuchunguza malisho na misitu karibu na nyumba yake. Alikuwa mtoto wa pekee nyumbani alikoishi na nyanya wake katika…